Muhnad al-Mayali alisema programu hizo ni za wafanyaziara wanaotembelea makaburi matukufu ya Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS) wakati wa maandamano ya Arbaeen, tovuti ya Al-Kafeel iliripoti.
Ameongeza kuwa ni sehemu ya mipango inayolenga kukuza na kuimarisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa watoto na vijana.
Yanafanyika katika msimu wa Arbaeen kwa mwaka wa nne mfululizo na ni pamoja na kozi za Qur'ani, mashindano, hotuba za elimu, nk, alibainisha.
Wakati huo huo, Majlisi ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu ambayo pia ina mfungamano na Mfawidhi wa na Haram ya Hazrat Abbas (AS), imezindua kituo cha kwanza cha Qur'ani kwenye njia ya wafanyaziara wa Arbaeen katika Jimbo la Babeli ili kuwafundisha usomaji sahihi wa Sura za Qur'ani.
Kwa mujibu wa Jawad al-Nasrawi, afisa wa baraza hilo, vituo 8 vya Qur'ani vile vile vitawekwa katika Mkoa wa Karbala.
Vituo vya Qur'ani vinaandaa vipindi vya usomaji wa Qur'ani, programu za elimu na mashindano kuhusu mafundisho ya Qur'ani na Kiislamu, aliongeza.
Mjumuiko wa maombolezo ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.
Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.
3489539